MAPATANO YA KIFO
Mtume Paulo katika barua yake ya pili kwa wathesalonike ,alitangulia kutabiri juu ya uasi mkuu ambao matokeo yake yangeleta kusimamishwa kwa uwezo wa Kipapa. Alitangaza kwamba siku ya Kristo haitakuja, “usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa yule mtu wa kuasi mwana wa uharibifu; Yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu, au kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Na zaidi ya hapo, mtume Paulo alionya ndugu zake wa imani kwamba “maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wathesalonike 2:3-4,7. Hata mwanzo wa nyakati hizo, aliyaona yakinyemelea kuingia kanisani, makosa ambayo yangeandaa njia kwa kukua kwa Upapa. Kidogo kidogo, kwanza kwa siri na kimya, na wazi zaidi ilipokuwa ikiongezeka kwa nguvu na kuyatega mawazo ya watu, “siri ya uasi” iliendeleza mbele udanganyifu wake na kazi yake ya makufuru. Mila za kipagani zikapata kuingia katika kanisa la Ukristo. Ile roho ya maafikiano na kufanana ilizuiliwa kwa muda lakini mateso makali yaliyolikuta kanisa yakafungulia upagani usio na kipimo! Lakini mateso yalipokoma, na Ukristo kuingia majumba ya wafalme, kanisa likaweka kando unyenyekevu wa Kristo na mitume wake kwa kujitakia makuu na kiburi ya makuhani na viongozi wa kishenzi; na katika sehemu ya sheria ya Mungu, badala yake likabadilisha elimu na mafundisho ya watu. Kuongoka nusu kwa Costantino, katika mwanzo wa karne ya nne, kulileta shangilio mkubwa; na ulimwengu, ukiwa umefunikwa mfano wa nguo ya haki, ukaingia kanisani. Sasa kazi ya uharibifu ikaendelea mbele kwa kasi. Ushenzi, ulipoonekana kushindwa, badala yake ukashinda. Roho wake akatawala kanisa. Mafundisho yake, sherehe zake, na mambo ya uchawi vikashirikishwa katika imani na ibada za wanaokiri kuwa Wakristo.
MTU WA KUASI
Mapatano hayo kati ya Upagani na Ukristo yalisababisha kustawi kwa yule “mtu wa kuasi” aliyetabiriwa katika unabii kuwa mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya Mungu. Utaratibu huu wa dini ya uongo ni kazi bora ya nguvu za Shetani. Ni nguzo ya juhudi yake yeye mwenye kukaa katika kiti kuitawala dunia kulingana na mapenzi yake. Shetani alijitahidi awali kufanya mapatano na Kristo. Alimjia Mwana wa Mungu katika jangwa la majaribu, akimwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wake wote, akamuahidi kutoa vyote mikononi Mwake ikiwa angekiri utawala wa huyu mfalme wa giza. Kristo alimkemea mshawishi huyo mwenye kiburi na kumfukuza. Lakini Shetani bado angali akileta majaribu hayo kwa mwanadamu. Kwa kupata faida za ulimwengu na heshima, Kanisa likaongozwa kutafuta upendeleo na dunia; na baada ya kumkana Kristo, likashawishika kutoa utiifu kwa mwakilishi wa Shetani yaani askofu wa Rumi.
MSINGI WA UPOTOVU
Ni mojawapo ya mafundisho tangulizi ya Kirumi ya kwamba papa ndiye kichwa halisi cha kanisa la Kristo ulimwenguni, ambaye amezingirwa na uwezo wa utawala juu ya maaskofu na wachungaji katika pembe zote za ulimwengu. Zaidi ya hayo, papa amepewa jina la Mungu. Amekuwa akiitwa kwa umbo la “Mungu Bwana Papa,” na amekuwa akinenwa kuwa asiyeanguka. Yeye hutaka watu wote wamsujudie. Dai lile lile Shetani alilosisitiza katika jangwa la majaribu, anaendelea kusisitiza kupitia Kanisa la Rumi, na idadi kubwa ya watu wako tayari kumtolea heshima. Lakini wamchao Mungu na kumheshimu huzingatia madai haya ya kujiinua juu ya Mbingu na ushawishi wa yule mjanja: “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Luka 4:8. Mungu hajawahi kudokeza katika Neno Lake ya kwamba Yeye amemteua mtu ye yote kuwa kichwa cha kanisa. Fundisho la utawala wa kipapa hupingana kabisa na mafundisho ya Maandiko. Papa hawezi kuwa na nguvu juu ya kanisa la Kristo ila tu kwa njia ya unyang’anyi. Warumi wamezusha kuwa Waprotestanti wamejitenga na katika kanisa la kweli. Lakini lawama hizi zina walenga hao wenyewe. Hao ndio walioishusha chini Kweli ya Kristo na wakajitenga na “imani iliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” Yuda 3. Kama vile Kristo alivyo kumbana na Vumbuzi la Uongo
Shetani alijua sawa kabisa ya yangewezesha watu kutambua udanganyifu wake na kupinga nguvu zake. Ni kupitia kwa Neno hilo Mwokozi wa ulimwengu alizipinga shambulizi zake. Katika kila shauri la yule adui, Kristo alitoa kinga la ukweli wa umilele, akisema, “imeandikwa.” katika kila shawishi la yule adui, Aliupinga akitumia hekima na nguvu ya Neno. Ili Shetani audumisha mvuto wake juu ya watu, na kusimamisha uwezo wa unyanganyi wa kipapa, ni mpaka angefanya wasiyajue Maandiko. Bibilia ingemwinua Mungu na kuwaweka wanadumu katika mahali pao halisi; kwa hivyo, kweli za Bibilia zingefichwa na kukanyagiwa chini. Na elimu hii ilibuniwa na Kanisa la Kirumi. Kwa mamia ya miaka usambazaji wa Bibilia ulikataliwa. Watu walikatazwa kusoma au kuwa nayo manyumbani mwao, na makuhani wasio na msingi na maaskofu wakatafsiri mafundisho yake ili kutosheleza ubinafsi wao. Kwa hivyo papa akawa Mungu duniani, ambaye amevikwa mamlaka juu ya kanisa na serikali kwamba Maandiko Matakatifu.
KUSUJUDU UPAGANI
Kinga ya ukweli ilipoondolewa, Shetani akafanya kulingana na mapenzi yake. Unabii ulikuwa umetangaza kwamba Upapa “ungefikiria kubadili majira na sheria. Ili kujipatia waumini kutoka kwa mataifa badiliko la ibada ya sanamu, na hasa kuinua Ukristo wao wa jina tu, ibada ya sanamu na makumbusho ya wafu iliingizwa pole pole katika ibada ya Wakristo. Amri ya kamati kuu mwishowe ikajenga utaratibu huu wa kuabudu sanamu. Ili kukamilisha kazi hii ya kukufuru, Rumi ikawazia kuiondoa kutoka kwa Sheria za Mungu amri ya pili, inayokataza uabuduji wa sanamu, na kugawanya amri ya kumi, ili waendelee kuwa na hesabu kamili.
MAPATANO YAFANYIKA
Kukubali mambo ya kidunia kuliendelea kufungua njia zaidi ya kupuuza uwezo wa Mbinguni. Shetani, akifanya kazi kupitia kwa viongozi waasi wa kanisa, wakaiharibu pia sheria ya nne, na kujaribu kuweka kando Sabato ya zamani, siku ambayo Mungu aliibariki na kutakasa (Mwanzo 2:2-3), na badala yake kuinua siku ya sherehe ilyokuwa inatunzwa na wamataifa kama “siku ya heshima ya juu.” Kwa mara ya kwanza badiliko hili halikujaribiwa dhahiri. Katika karne za kwanza Sabato ya kweli ilitunzwa na Wakristo wote. Walikuwa na wivu kwa heshima ya Mungu, na, wakiwa na imani ya kwamba sheria yake, ni imara, kwa juhudi wakatunza usafi wa maagizo yake. Lakini kwa ujanja mwingi Shetani akafanya kazi kupitia kwa wawakilishi wake ili kutimiza lengo lake. Ili mawazo ya watu yapate kuvutwa kwa Jumapili, ikafanywa kuwa ni siku ya sherehe kwa kuheshimu ufufuo wa Kristo. Mikutano ya kidini ilifanywa katika siku hiyo; na huku siku hiyo ikitunzwa kama siku ya maburudisho, laikini Sabato pia ikiendelea kutunzwa. Kwa kuiandaa njia ya kazi yake alioipanga kuikamilisha, Shetani kabla ya kurudi kwa Kristo, alikuwa amewaongoza Wayahudi, kuibebesha Sabato kwa maagizo magumu, na kufanya utunzaji wake kuwa mzigo. Na sasa, ili kuipa nafasi ile nuru ya uongo aliyokuwa ameibuni na kuwaaminisha wengi, akatoa dhihaka juu Sabato akiita eti ni sheria ya Wayahudi. Wakristo walipoendelea kutunza Jumapili kama sherehe ya furaha, akawaongoza, ili apate kuwaonyesha uadui dhidi ya Wayahudi, kwa kuifanya Sabato kuwa siku ya kufunga, huzuni na siku ya utusitusi.
BADILIKO MATHUBUTI
Mwanzo wa karne ya nne mfalme Costantino alipitisha sheria ya kuifanya Jumapili kuwa ya sherehe ya wote katika enzi ya Kirumi. Siku ya jua iliheshimiwa na wafuasi wa kipagani na Wakristo pia; zilikuwa hila za mfalme kuunganisha Wakristo. Alisukumwa kufanya hili na maaskofu wa kanisa, waliokuwa na tamaa na kiu ya utawala, wakifikiria ya kwamba siku hiyo ikiabudiwa na wote Wakristo na watu wa mataifa, ingeinua kukubalika kwa ukristo wao wa uliochanganyika na upagani na kwa hivyo kuendeleza uwezo na utukufu wa kanisa. Lakini wengi wa Wakristo wacha Mungu walisukumwa pole pole kuitakasa Jumapili kama siku takatifu, na pia waliishikilia Sabato ya kweli kuwa takatifu kwa Bwana, na wakaitunza kulingana na utiifu wa amri ya nne. Mdanganyifu mkuu hakuwa amemaliza kazi yake. Alinuia kukusanya ulimwengu wa Wakristo chini yake na kudhihirisha nguvu zake kupitia kwa huyo mdanganyifu anayedai kuwa mwakilishi wa Mungu duniani, askofu huyo mwenye kiburi anayedai kuwa mwakilishi wa Kristo. Kupitia kwa wapagani walioongoka nusu, maskofu wenye tamaa, na watu wa kanisa waupendao ulimwengu Shetani akalikamilisha kusudi lake. Mikutano mikubwa ilifanywa mara kwa mara, ambayo wakuu wa kanisa walikusanyika kutoka ulimwenguni kote. Na katika kila kikao Sabato iliyowekwa na Mungu ilishushwa chini kidogo kidogo. huku Jumapili ikiinuliwa juu. Kwa hivyo siku ya sherehe ya kipagani ikaja kutukuzwa na kuheshiwa kama siku takatifu, huku Sabato ya Bibilia ikakanyagiwa chini kuwa mabaki ya Wayahudi, na walioendelea kuiabudu wakatangazwa kuwa wamelaaniwa. Kuondolewa kwa Muhuri wa Muumbaji
MUASI MKUU alishinda kwa kujiinua mwenyewe “kwa cho chote kiitwacho Mungu, au kuabudiwa.” 2 Thesalonike 2:4. Amejaribu kubadili amri ya pekee katika sheria za Mungu ambayo dhahiri inawaelekeza watu kwa Mungu wa kweli aishie. Katika sheria ya nne, Mungu amedhihirishwa kama Muumbaji wa mbingu na nchi,na hivyo basi kubainishwa kutoka miungu mingine ya uongo. Ilikuwa ni ya kumbukumbu ya kazi ya Umbaji iliyo siku ya pumziko kwa mwanadamu. Lilikuwa ni kusudi la Mungu kuhifadhi daima katika mawazo ya wanadamu muumbaji wa viumbe vyote anayestahili pekee heshima na lbada. Shetani amekuwa daima akipigana vita kuwageuza watu kutoka kwa utiifu wao kwa Mungu, na utiifu kwa sheria Zake; hivyo basi anaelekeza juhudi zake hasa juu ya sheria inayomwonyesha Mungu kama Muumbaji. Madhehebu ya Waprotestanti yanasisitiza kuwa kufufuka kwa Kristo katika siku ya Jumapili ndio ilifanya siku hiyo kuwa Sabato ya Wakristo. Lakini hapo hakuna ushahidi wa Maandiko. Kristo wala wanafunzi wake hawakutoa heshima kwa siku hiyo.